Imekuwa kama miujiza au tuseme ni mizimu imechukia mara baada ya kumsulubu mtani? Amini usiamini... Simba ya Tanzania imeondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mikwaju ya penati 9-8.
Kipindi cha kwanza kilimalizika timu zote zikitoka sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili sekunde ya 23 walikuwa Al Ahly Shandy wenye ngekewa kuianza safari ya kupunguza magoli waliyochapwa wakiwa bongo nao bila ajizi ndani ya dakika 24 walikuwa tayari wamelipa deni kupitia makosa ya udhaifu wa ngome ya Simba, hadi dakika 90 zinamalizika simba ilikuwa imefungwa 3-0.
Ndipo time ya maamuzi mikwaju ya penati kwa mujibu wa kanuni za mashindano ikawadia.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam Simba ilishinda magoli 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika (CAF) vizuri.
Hata hivyo imeshindwa kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment