Tuesday, May 15, 2012

JB AELEZA ALIVYOKWEPA KUUAWA NA MAJAMBAZI


Na Imelda Mtema
MCHEZA filamu anayetamba kwenye ‘game,’ Jacob Steven ‘JB’ (pichani) hivi karibuni alinusurika kuuawa na majambazi waliovamia Pub ya msanii mwenzake, Aunt Ezekiel iliyopo eneo liitwalo Gereji Mwananyamala jijini Dar.
Akizungumza na Ijumaa, JB alisema kuwa baada ya majambazi hao kuvamia katika pub hiyo saa 5.30 usiku, hakuwastukia kama walikuwa wahalifu bali alidhani ni wateja wa kawaida.
“Mimi sikuwashitukia kama wale watu walikuwa majambazi, ila baada ya kutoa bastola na kutuamuru tulale chini na tutoe kila kitu nikajua kimenuka, nikatimua mbio ambazo sijawahi kukimbia licha ya mwili wangu huu,” alisema JB.
Aliongeza kuwa, wakati akitimua mbio aliwasikia watu wakimuaru asimame lakini hakutii hadi alipofika Kituo cha daladala cha Komakoma ndipo alisimama na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru na kifo.
Mei 7, mwaka huu usiku, majambazi kadhaa waliivamia pub ya Aunt Ezekiel na kufanikiwa kupora fedha na kumjeruhi mkononi na mgongoni kwa risasi kijana mmoja aitwaye Musa mkazi wa Sinza.

No comments:

Post a Comment