Manchester United wameendelea kuweka ndoto zao za kutetea ubingwa wao kwa kuichapa Swansea kwa mabao 2-0.
United walijitahidi kutaka kufunga mabao mengi
ili kupunguza tofauti iliyopo kati yao na Manchester City, lakini
walipoteza nafasi nyingi za kufanikisha hilo.Paul Scholes ndio aliandika bao la kwanza la United huku la pili likifungwa na Ashley Young.
Manchester City wanaendelea kuongoza ligi wakiwa pointi sawa na United, lakini wana magoli 8 zaidi.
Manchester City watatangazwa kuwa mabingwa wiki ijayo iwapo wataichapa QPR, hata kama Manchester United watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland.
Iwapo United watataka kuchukua ubingwa, watalazimika kupata ushindi wa magoli zaidi ya manane huku wakizingatia matokeo yatakayopatikana kati ya City na QPR.
No comments:
Post a Comment