Sunday, May 20, 2012

Chelsea mabingwa wapya Ulaya 2012

Drogba

Mkwaju wa Drogba umeipa ushindi Chelsea

Chelsea ya England imeshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya 2012 baada ya kuwashinda Bayern Munich ya Ujerumani kwa mikwaju ya penati 4-3.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 za kawaida na kulazimika kwenda katika dakika za nyongeza. Hata hivyo timu hizo ziliendelea kuwa sare na hivyo kulazimika kuamiliwa kwa mikwaju ya penati.

Awali, Thomas Muller alindika bao la kwanza kwa Bayern Munich katika dakika ya 83, lakini Didier Drogba alisawazisha kwa mpira wa kichwa katika dakika ya 88.

Mchezo uliendelea katika muda wa ziada na dakika nne za kipindi cha kwanza Drogba alimfanyia faulo Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na kusababisha penati. Arjen Robben alipiga penati hiyo lakini ilidakwa na kipa Petr Cech.

No comments:

Post a Comment