Monday, May 21, 2012

Tetemeko la ardhi Italia yaleta maafa makubwa


Maelfu ya watu walioachwa bila makao kufuatia tetemeko kubwa la ardhi Kaskazini mwa Italia watalazimika kulala kwenye mahema kufuatia wasiwasi wa kuzuka tetemeko jingine.
Watu sita walifariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika tetemeko hilo la ardhi lililotokea Jumapili.
Serikali imetoa mahema mengi kwa wananchi hao walioathirika na tetemeko la ardhi ingawa wengine wameamua kulala katika magari yao.
Wataalamu walisema tetemeko hilo lilifikia kipimo ya Richa 6.
Waziri Mkuu wa Italia, Mario Monti, atakatiza mkutano wake na viongozi wenzake wa NATO unaoendelea Marekani kwa ajili ya hali ilivyo nchini mwake.

No comments:

Post a Comment