Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakifika Kituo cha Polisi Iringa. |
Washtakiwa
wakishuka kwenye Karandinga kuingia rumande baada ya kukosa dhamana
kutokana na wajeruhiwa wawili kati ya wale watatu kuwa katika hali
mbaya hospitali ya mkoa wodi namba 5.
|
Wafuasi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Manispaa ya Iringa
wakitokea Mahakamani kuelekea Kituo cha Polisi Iringa wakienda kutaka
kupata maelezo juu ya Mlalamikiwa Mh. Diwani Idd Chonanga ambaye ndiyo
mlalamikiwa wa kwanza kutofikishwa Mahakamani baada ya kukamatwa na
Polisi na kuachiwa kwa dhamana.
(Picha zote na Said Ng'amilo-Mdau wa Mjengwa Blog Iringa)
HATMA YA MAANDAMANO YA WAFUASI WA CHADEMA
Kaimu
Kamanda wa Mkoa akiri kutofikishwa kwa Mh. Diwani Idd Chonanga
mahakamani leo kwa kuwa aliachiwa kwa dhamana jana katika kituo cha
Polisi na kuahidi Mh. Huyo atafikishwa mahakamani kesho tarehe
16/05/2012. Maelezo hayo alipewa Mheshimiwa Mbunge wa Iringa Mjini
Peter Msigwa (Chadema) baada ya kuonana na Kaimu Kamanda ofisini kwake
leo.
|
No comments:
Post a Comment