Wednesday, May 9, 2012

Mwingereza matatani kwa ugaidi Kenya


Jermain Grant
Raia wa Uingereza ambaye ni mwislamu na mwenye msimamo mkali amefikishwa katika mahakama moja mjini Mombasa, Kenya .
Jermaine Grant mwenye umri wa miaka 29 , alitiwa mbaroni mwezi Disemba mwaka jana kwa tuhuma za kupanga mashambulizi ya bomu pamoja na kumiliki vilipuzi kinyume cha sheria.
Maafisa wa serikali ya Kenya wanasema raia huyo kutoka London, ana uhusiano na kundi la wapiganaji la Al Shabab nchini Somalia, ambaye pia aliwahi kufungwa nchini humo kwa kutokuwa na kibali cha kuingia nchini.
Anashtakiwa pamoja na wenzake watatu ambao ni raia wa Kenya ambapo amekana tuhuma zinazomkabili.
Mwandishi wa BBC aliyepo Mombasa Gabriel Gatehouse ,anasema Grant amefika mahakamani akiwa ametulia.
Waandishi wa habari walifurika katika mahakama hiyo na haikujilikana kama kesi hiyo inaweza kuendelea.
Inaarifiwa kesi yenyewe ingali inakumbwa na utata.
Grant alitiwa mbaroni kwa mara ya kwanza mwaka 2008 katika eneo la mpaka waKenya na Somalia lakini alitoroka wakati alipokuwa mahabusu katika kituo cha polisi.
Duru zinaarifu mtuhumiwa alitoroshwa kutoka kituo cha polisi na kundi la Al Shabab.

No comments:

Post a Comment