Manchester City imechukua tena usukani wa ligi kuu ya England na kuongeza matumaini ya kunyakua ubingwa baada ya kuwachapa mahasimu wao Manchester United kwa 1-0.
Manchester City sasa wanaongoza ligi licha ya kuwa na pointi sawa na Man United, lakini wana idadi kubwa ya magoli.
Ushindi huu wa aina yake umekuja wakati ndoto za Manchester City za kuchukua ubingwa zikiwa zimekwisha fifia baada ya kufungwa na Arsenal mwanzo wa mwezi Aprili huku United wakiongoza kwa pointi nane.
Ligi hii huenda ikamalizika kwa chachu kubwa katika michezo miwili iliyosalia ambayo timu zote hazina budi kushinda iwapo zinataka kuweka matumaini ya kunyakua ubingwa.
Man City watakwenda kupambana na Newcastle kabla ya kuikaribisha QPR, huku United wakicheza na Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford kabla ya kusafiri kupambana na Sunderland katika mchezo wa mwisho wa ligi.
No comments:
Post a Comment